Feature

Je! utaenda kufanya mapumziko ya Krismasi ndani ya meli? Hii hapa taarifa unayo hitaji.

Baada ya Meli kwa jina la Ruby Princess kuleta mamia ya kesi za UVIKO mjini Sydney katika mwaka wa 2020, Meli ya the Majestic Princess imerudia historia iliyo kuwa imerekodiwa katika siku za nyuma. Kufanya likizo baharini kwa sasa huja na orodha ya ziada ya usalama. Endelea kusoma kupata taarifa.

Cruise and COVID.jpg

Koa and Sara have long awaited their postponed cruise trip. But is it still safe to go on a cruise? Credit: Yuya Jingu

Key Points
  • Cruise companies and Australian government develop protocol to mitigate COVID spread
  • Be up-to-date with COVID vaccination before travel
  • Check ventilation of cruise ship and use good quality face mask
Emi Jingu ni mkaazi wa Sydney, yeye na familia yake wamekuwa wakitazamia likizo yao ndani ya meli mwaka ujua. Iliwabidi wafute mipango yao katika mwaka wa 2020 na pia 2021.

“Nitakuwa nina danganya nikisema sina wasiwasi kuhusu kupata UVIKO ndani ya meli. Ila furaha yakusafiri ndani ya meli kama familia ni muhimu sana," mama huyo wa watoto wawili alisema.

Tangu wakati serikali ya shirikisho ilipo ondoa vizuizi vya meli kuingia nchini Australia mnamo Aprili mwaka huu, maambukizi ya UVIKO yameripotiwa ndani ya meli kama Coral Princess, hali inayo tukumbusha meli ya Ruby Princess katika mwaka wa 2020, ambako maisha 28 yalipotezwa na zaidi ya watu 660 waliambukizwa.

Hata hivyo, "hali ilikuwa tofauti sana" wakati huo, amesema Profesa wamagonjwa katika chuo cha Kusini Australia Adrian Esterman.

“Hatuna chanjo au dawa zakupambana na virusi na hapakuwa chochote kwa upande wa kinga. Siku hizi, kama mamia ya abiria waliombukizwa wanashuka kutoka meli, haitakuwa na tofauti kubwa katika maambukizi ya jamii katika sehemu ambako wanashukia" ame elezea.

“Hata hivyo, sikitu kizuri kuugua ukiwa katika likizo ndani ya meli, na abiria walio ambukizwa wana weza salia na matatizo ya afya ya muda mrefu," Prof Esterman ame ongezea.
COVID MAJESTIC PRINCESS CRUISE SHIP
The Ruby Princess COVID outbreak of 2020 led to a ban on cruiseships which was lifted only this year. Source: AAP / DEAN LEWINS/AAPIMAGE

Mafunzo kutoka meli ya Ruby Princess

Serikali ya Australia, pamoja namakampuni yameli, wametengeneza itifaki zaku kabiliana na maambukizi ya UVIKO baada ya sakata la meli ya Ruby Princes.

Serikali ya New South Wales nayo imechapisha taarifa kuhusu hatari za UVIKO, kuhusiana na vyombo vinavyo kuja jimboni kupitia mfumo wao wa Tier.

“Chamuhimu pengine ni hewa safi na makampuni mengi ya meli yame karabati mifumo yakusambaza hewa kwa kujumuisha vichungi kwa jina la HEPA pamoja nakupitisha hewa safi mara kwa mara ndani ya vyumba," amesema Prof Esterman.

Abiria wanaweza pata taarifa kutoka makampuni ya meli, kama wameboresha mifumo yao yakusambaza hewa safi pamoja na hatua zingine za usalama wa UVIKO-19.

“Mara nyingi taarifa hiyo itakuwa kwenye tovuti zao," ameongezea.

Usiabiri kama una umwa

Wasafiri wanao kuja nakutoka Australia, silazima watoe thibitisho za chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Hata hivyo, Idara ya Afya na Huduma yawazee imependekeza uzingatie safari ndani ya Meli kama hauja pata chanjo zako zote. Vile vile, kama uko katika hatari zaidi yakupata ugonjwa mubaya ukiambukizwa UVIKO-19.

Wale ambao wana dalili au wame patwa na UVIKO-19 wiki moja kabla ya safari, hawastahili abiri meli kwa sababu wanaweza kuwa "chombo cha ugonjwa wowote UVIKO ukijumuishwa," wataalam wameonya.

"Abiria hupakizwa katika sehemu ndogo na virusi husambaa kwa viwango vya juu," amesema Prof Esterman.
Cruise Sara.jpg
Passengers spend days together on a cruiseship in a constrained space leading to a higher risk of infection. Credit: Emi Jingu
Bi Jingu na familia yake wame pata chanjo kamili.

“Nadhani chenye tunaweza fanya nikupunguza kutoka kabla ya safari yetu nakuvaa barakoa kila wakati kupunguza hatari yakuambukizwa," alisema.

Familia hiyo imejipa pia bima maalum ya safari ndani ya meli, inayo funika safari hiyo pamoja na shughuli zitakazo fanywa katika nchi kavu.

Prof Esterman amewakumbusha wanao safiri kwa meli wakati huu wa msimu wa likizo, wahakikishe wamepata chanjo kamili.

"Bado ni kinga bora dhidi ya magonjwa mabaya," ameshauri.

“Vaa barakoa nzuri usoni (KN95/N95/P2) wakati wote ukiwa ndani. Hakikisha unabima ya safari inayo funika UVIKO. Uki ugua vibaya, utahitaji ondolewa katika meli hiyo kwa ajili yamatibabu," ameongezea.

Serikali ya New South Wales ime unda orodha yakufuatilia kwa wanao panga kusafiri kwa meli.

Kwa taarifa zaidi, tembelea Idara ya Afya na Huduma ya wazee na pamoja na ushauri wa .

SBS ina nia yakutoa taarifa mpya za UVIKO-19 kwa jamii zenye tamaduni na lugha tofauti nchini Australia. Baki salama na endelea kupata taarifa kwa kutembelea mara kwa mara 

Share
Published 30 November 2022 11:25am
Updated 1 December 2022 11:30am
By Yumi Oba
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends