Latest

'Mwanzo wa wimbi lingine': Tunajua nini kuhusu aina za UVIKO za XBB na BQ.1?

Mamlaka wa afya wa Australia wako katika hali ya tahadhari wakati ushahidi ambao haujathibitishwa kupitia utafiti umedokeza kuwa XBB na BQ.1 zinachangia katika ongezeko ya kesi mpya za UVIKO kwa mara ya kwanza katika wiki tatu.

NSW CORONAVIRUS COVID19

Healthcare workers administer COVID-19 PCR tests at the St Vincent’s Drive-through Clinic at Bondi Beach in Sydney. (file) Source: AAP / BIANCA DE MARCHI/AAPIMAGE

Key Points
  • XBB and BQ.1 can escape immunity from past infection and vaccination: Victorian Chief Health Officer
  • New variants don't cause severe illness than other Omicron subvariants: WHO
  • Vaccines still work but may have reduced protection against new subvariants: WHO
Majimbo mengi ya Australia pamoja na wilaya, ziliripoti ongezeko kwa kesi za kila wiki za UVIKO-19 katika wiki iliyo isha na 28 Oktoba.

Tasmania iliripoti ongezeko kubwa zaidi la kesi la asilimia 30.

Jimbo hilo lilifuatwa na Australian Capital Territory (26. 25%), Victoria (24.4%), Magharibi Australia (18%), New South Wales (13%) na Kusini Australia (10%).
Afisa Mkuu wa Afya wa Victoria Brett Sutton, amesema XBB na BQ.1 kwa sasa zinachangia kwa takriban asilimia 10 yakesi zote katika jimbo hilo, na inaweza pita aina dogo sugu ya BA.5.

"Viashiria hivi (vikijumuishwa na asilimia nane ya ongezeko kwa tiba za virusi) inaonesha tuko katika mwanzo wa wimbi lingine la UVIKO-19," Bw Sutton alisema Ijumaa.

Alisema aina hizo za virusi zina ongezeka kesi nyingi pamoja na wimbi za visa vyakulazwa hospitalini kwa sababu ya uwezo wao waku kwepa kinga kutoka maambukizi ya zamani (virusi vya BA.5 vikijumuishwa) na udhaifu wa kinga kutoka chanjo za zamani.

Idara ya Afya ya NSW nayo imesema inafuatilia kwa karibu, ujio wa virusi aina ya XBB na BQ.1 pamoja na data zingine zakimataifa naza nchini, kuchunguza uwezekano wa ukuaji wa virusi vipya.
Aina za virusi za XBB na BQ.1 ni gani?

XBB ni mchanganyiko wa virusi vya BA.2.10.1 na BA.2.75. Ina maambukizi yakimataifa ya asilimia 1.3 na imetambuliwa katika nchi 35.

BQ.1 ni aina yakirusi BA.5 chenye maambukizi yakimataifa ya asilimia 6. Imepatwa katika nchi 65.

Ukali

Catherine Bennett ni mtaalam wamagonjwa, amesema aina hizi zamaambukizi hazionekani ni kama zinasababisha magonjwa mabaya.

"Ila wasiwasi ni kwamba ni tofauti sana na (virusi vingine vya Omicron) kuwa na uwezo wakinga kukwepa," Profesa Bennett alieleza shirika la habari la SBS.

"Hii ina maana kuwa maambukizi ya hivi karibuni pamoja na aina nyingine ya Omicron, haitaweza toa kiwango sawia cha ulinzi dhidi ya maambukizi."
Professor Catherine Bennett.
Deakin University chair of epidemiology Professor Catherine Bennett. Source: Supplied / Supplied by Professor Catherine Bennett
Shirika la Afya la Dunia (WHO) lina amini kuwa XBB na BQ.1 sitofauti sana na chimbuko la Omicron kuzingatiwa kuwa aina mpya ya kirusi inayo zua wasiwasi.
Data ya sasa haidokezi kuna utoafuti mkubwa, kwa ukali wa ugonjwa kutokana na maambukizi ya XBB
"Kuna ushahidi wa mapema unao tunga kidole kwa kiwango cha juu cha hatari yakuambukizwa tena, badala ya vizazi vingine vinavyo zunguka vya Omicron. Kesi zakuambukizwa tena kimsingi zilikuwa zimedhibitiwa kwa wale ambao walikuwa na maambukizi kwanza kabla ya wakati wa Omicron."

WHO ilisema BQ.1 inaonesha faida kubwa ya ukuaji kuliko aina zingine za Omicron ambazo ziko Ulaya na Marekani na zinastahili kufuatiliwa kwa karibu.
Kuna uwezekano wa hatari kubwa yakuambukizwa tena, ambayo inahitaji uchunguzi wa ziada.
"Hata hivyo, kwa sasa, hakuna data ya magonjwa yakudokeza kuna ongezeko katika ukali wa ugonjwa," ilisema.

Je! chanjo za sasa ni fanisi dhidi ya aina mpya ya virusi?

WHO imesema kinga kutoka chanjo inaweza pungua. Bado hakuna madhara makubwa kwa ulinzi dhidi ya ugonjwa mkali unao tabiriwa.

Prof Bennett amesema ni mhimu kwa kila mtu achukue chanjo za jeki zilizo pendekezwa, haswa kwa wale amboa wana zaidi ya miaka 50 au wana magonjwa sugu.

"Chanjo za jeki zimeonekana hutoa kinga ya muda mfupi dhidi yakupata maambukizi," alisema.

Wimbi zakimataifa za XBB na BQ.1

Prof Bennett amesema aina hizo za virusi zime sababisha ongezeko ya kesi mpya ila, sikama katika wimbi za nyuma.

"France ilikuwa na viwango vya juu zaidi vya virusi vya BQ.1 mapema Oktoba na, inaonekana kama viwango vyao yakulazwa hospitalini nikama vime anza pungua, kwa hiyo hali hiyo inatia moyo," alisema.

"Hali ni hivyo pia nchini Singapore kwa XBB."
Kinga na hatua zakuzuia dhidi ya aina mpya yamaambukizi

Prof Bennett amesema uwezekano wa wimbi mpya hupungua wakati watu wanajumuika zaidi nje.

Profesa Sutton aliwakumbusha wakaaji kuwa chanjo, barakoa, hewa safi, vipimo nakubaki nyumbani unapo umwa pamoja na tiba za UVIKO-19 ni fanisi sana kupunguza usambaaji wa virusi na magonjwa.

"Kama haupimwi, hauwezi pata tiba mhimu, zinazo jumuisha tiba zakukabiliana na virusi," alisema.

SBS ina nia yakutoa taarifa mpya za UVIKO-19 kwa jamii zenye tamaduni na lugha nyingi za Australia. Endelea kuwa salama na endelea kupata taarifa kwa kutembelea mara kwa mara

Share
Published 31 October 2022 4:07pm
By Sahil Makkar
Presented by Gode Migerano
Source: SBS


Share this with family and friends