Taarifa ya Habari 23 Aprili 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu amewasifu wanajeshi wa Australia walio kuwa sehemu ya historia ya jeshi, katika eneo la Kokoda Track anapo jiandaa kutembea katika nyayo zamagwiji.


Anthony Albanese anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa kwanza aliye madarakani, atakaye tembea katika njia hiyo ya milima Papua New Guinea, kuanzi leo Jumanne na tamati itakuwa katika ibada ya alfajiri ya siku ya Anzac Alhamisi.

Mtandao wa jamii wa X wa Bilionea Elon Musk, ume amuriwa kuwazuia watumiaji wote kutazama video zinazo husiana na madai ya shambulizi la kigaidi katika kanisa moja mjini Sydney. Bw Musk na kampuni yake wali zua hoja ya uhuru wakujieleza pamoja na maswala ya amri ya mamlaka kutoka mdhibiti wa intanet wa Australia, kuhusu kuondolewa kwa video za tukio la 15 Aprili. Video mbaya zaku kera zime fungiwa kwa watu wanao ishi Australia. X imesema ilikuwa ime fuata maagizo yakuziondoa ila, ime pinga hali yao yakimataifa, ikisema kamishna wa eSafety haina mamlaka kama hayo.

Ripoti mpya imepata ndota ya Australia yakumiliki nyumba yako, ime vunjwa kwa ongezeko za kodi pamoja na bei zaku nunua nyumba zilizo panda sana. Baada yakufanyia tathmini zaidi ya matangazo elfu 45 ya nyumba zaku kodi, ripoti ya Anglicare Australia kwa uwezo waku kodi nyumba imesema soko iko katika hali mbaya kuliko kabla. Ripoti hiyo imeongezea kuwa viwango vya nyumba zilizopo zakukodi kitaifa, imekuwa chini kwa 0.7%, wakati kodi za nyumba wastan zimeongezeka kufika $200 kila wiki kuliko ilivyo kuwa kabla ya janga la UVIKO-19.

Mafuriko makubwa yameyakumba maeneo mengi ya Afrika Mashariki ambayo yanakabiliwa na mvua za mfululizo, Burundi ikiomba msaada wa kimataifa wa kuisaidia kupambana na maafa hayo. Maji katika Ziwa Tanganyika yameongezeka na kusababisha mafuriko katika bandari ya Bunjumbura, biashara zimevurugika katika mji mkuu wa kiuchumi na katika maeneo mengine yanayotegemea kwa kiwango kikubwa msaada kutoka wafadhili. Raia wa Burundi walikuwa wakihangaika kukabiliana na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha nchini humo, huku maelfu ya watu wakikosa makazi na nyumba nyingi na shule kuharibiwa.

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak ameahidi leo Jumatatu kuanza kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda ndani ya wiki 10 hadi 12, akiliambia bunge kwamba atailazimisha sheria hiyo mpya kupita licha ya upinzani uliopo. Sunak alisema serikali imekodisha ndege za kibiashara na imewapatia mafunzo wafanyakazi ili kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda, ikiwa ni sehemu ya sera anayotarajia itakiimarisha chama chake cha Conservative kabla ya uchaguzi baadaye mwaka huu. Hakuna kama, au lakini, ndege hizi zinakwenda Rwanda, Sunak aliwaambia waandishi wa habari.

Utawala wa Kaunti ya Samburu sasa umeamua kugeukia maombi kama njia ya kukomesha ujangili ambao umesababisha vifo vya raia wengi wakiwemo maafisa wa usalama. Visa vya wizi wa mifugo, mashambulio na uharibifu wa maji vimevuruga hali ya maisha katika kaunti hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Baada ya juhudi za maafisa wa usalama za kukomesha hali hii kutozaa matunda, Gavana wa Samburu, Lati Lelelit, sasa anaandaa maombi yanayoshirikisha makanisa mbalimbali na viongozi wa eneo hilo kuombea amani.

Share