Jinsi yaku saidia wanyamapori walio jeruhiwa nchini Australia

Exploring Stradbroke Island near Brisbane

Stradbroke Island in Queensland, Australia Source: iStockphoto / Kevin LEBRE/Getty Images/iStockphoto

Australia ni nyumbani kwa baadhi ya wanyamapori wa aina mbalimbali na wanaovutia duniani, matokeo ya kutengwa kwa Australia kama bara na historia yakipekee ya mageuzi ambayo yametokea kwa ma milioni ya miaka.


Kama unasafiri au unafanya ziara nchini Australia, kuna uwezekano mkubwa waku kutana na baadhi ya aina zetu zakipekee za wanyapori.

Kwa bahati mbaya, wakati mwingine wanyamapori huugua au, wanaweza jeruhiwa namagari, miundombinu au katika majanga yakiasili kama mioto ya vichaka au mafuriko. Kwa hiyo unastahili fanya nini uki kutana na wanyamapori walio jeruhiwa au wanao ugua?

Kutegemea na unako ishi nchini Australia, aina ya wanyamapori utakao waona wata tofautiana kulingana na mazingira, hali ya hewa na makazi.

Kuna aina nyingi ya ndege, na wanyama wanao jumuisha aina ya nyoka wenye sumu na wasio na sumu nchini Australia.

Katika kanda za kaskazini, unaweza waona wanyamapori kama kangaroos, crocodiles, na cassowaries. Katika maeneo makavu ya magharibi kuna wanyama pori kama emus, red kangaroos na ndege wazuri wa jangwani.

Na katika kanda za kusini unaweza waona wanyamapori kama possums, wombats, wallabies, na aina ya glider, au hata seals, penguins pamoja na Tasmanian devils wanao patikana katika eneo la Kusini south Tasmania.

Kujua chakufanya unapo kutana na wanayapori ambao wame umia au wame ugua ni mhimu, ili ujue jinsi bora yaku wasaidia wakati unahakikisha usalama wao, ili wanyamapori hao wawe na nafasi bora yakupata matibabu nakupona.

Share