Taarifa ya Habari 15 Aprili 2024

City - Swahili.jpg

Polisi wamesema mwanaume aliye uwa watu sita kwa kuwadunga kisu ndani ya soko la Westfield Bondi Junction, ali waepuka wanaume kimakusudi nakuwalenga wanawake na watoto.


Waathiriwa tano kati ya sita walio uawa katika shambulizi hilo walikuwa wanawake pamoja na mlinzi mmoja wakiume, hali iliyofanya vyombo vya habari kumhoji Kamishna wa Polisi wa New South Wales Karen Webb, kama matendo ya mhalifu yali sababishwa na jinsia. Watu sita wali uawa baada ya mwanaume kutoka Queensland, Joel Cauchi kufanya shambulizi la kisu ndani ya soko hilo la Westfield.

Takriban $18 milioni zimetumwa maramoja katika ofisi ya mchunguzi wa vifo ya New South Wales, kuanzisha uchunguzi huru wa vifo kuhusiana na shambulizi la kisu ndani ya soko la Bondi Junction. Kiongozi wa New South Wales Chris Minns hii leo [[Jumatatu April 15]] alifanya tangazo hilo, akisema tume hiyo itakuwa na wafanyakazi na rasilimali pamoja na naibu mchunguzi wa vifo wa jimbo ata teuliwa kwa chunguzi zote zakisayansi, zinazo fanyika wakati wa uchunguzi huo wa umma.

Waziri Mkuu Anthony Albanese amejiunga na viongozi wengine wa dunia, kukosoa shambulizi la Iran dhidi ya Israel. Usiku wakuamkia Iran ili tuma mamia ya ndege zisizo na rubani zenye mabomu pamoja namakombora Israel, katika kile kinacho dhaniwa kuwa ni jibu kwa shambulizi la ubalozi wa Iran nchini Syria mapema mwezi huu. Watu kumi na mbili wali uawa Aprili mosi, majenerali wawili wakijumuishwa, Iran ililaumu Israel kwa shambulizi hilo. Israel haija dai uwajibikaji kwa shambulizi hilo.

Na walinzi wa watumiaji, vyama vya wafanyakazi pamoja na watoaji wa mboga wametoa malalimishi yao ndani ya Seneti leo, Aprili 15 wametoa makaripio makali kwa masoko mawili makubwa. Wakati gharama ya maisha inaongezeka, na bei za mboga zinapo endelea kuongezeka sambamba na faida za masoko makubwa, makundi kadhaa yanatumia vikao hivyo vya seneti kwa bei zamasoko kuelezea wasiwasi wao.

Takriban watu 12 waliuawa na zaidi ya 50 bado hawajulikani walipo, baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi kwenye mto kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa wa eneo hilo, na kiongozi wa shirika la kiraia walisema Jumapili. Maporomoko hayo yalitokea Jumamosi adhuhuri katika wilaya ya Dibaya Lubwe katika jimbo la Kwilu, na kusababisha udongo na uchafu kwenye ukingo wa Mto Kasai, ambapo boti moja ilikuwa ikitia nanga, na watu walikuwa wakifua nguo.

Mwanamke wa Rwanda, aliyeondolewa Marekani, miaka mitatu iliyopita amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo, gazeti la The New Times limeripoti Jumamosi. Mahakama katika mji wa kusini wa Huye ilimtia hatiani Beatrice Munyenyezi, mwenye umri wa miaka 54 kwa mashtaka ya uhalifu wa mauaji ya kimbari katika kushiriki, kuchochea kutekelezwa mauaji na kushiriki ubakaji. Hata hivyo hakutiwa hatiani kwa mashaitaka ya kupanga mauaji ya kimbari, gazeti la kitaifa la Rwanda limeandika.

Share