Taarifa ya Habari 18 Aprili 2024

City - Swahili.jpg

Askofu aliye dungwa kisu wakati wa ibada iliyo kuwa ikipeperushwa mubashara, amezungumza kwa mara ya kwanza tangu shambulizi hilo linalo shukiwa kuwa lakigaidi, akisema ame msamehe kijana anaye shukiwa kuwajibika kwa shambulizi hilo.


Shambulizi hilo dhidi ya askofu Mar Mari Emmanuel wa kanisa laki Assyrian, lilifanyika ndani ya kanisa la Christ the Good Shepherd Church ambalo liko katika kitongoji cha Wakeley, Magharibi Sydney usiku wa Jumatatu. [[April 15]] Mvulana mwenye miaka 16 amekamatwa kuhusiana na tukio hilo ila, bado haja funguliwa mashtaka na anaendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi hospitalini. Katika ujumbe wa sauti ulio tolewa na kanisa hilo hii leo Alhamisi 18, Askofu huyo alisema ana endelea vizuri na anapona haraka, wakati huo huo amewaomba waumini wake watii sheria baada ya mgomo kutokea punde baada ya shambulizi hilo. Askofu huyo ameomba utulivu, naku wahamasisha watu watii sheria na washirikiane na miongozo ya jeshi la polisi. Wito huo umejiri baada yaku kamatwa kwa mwanaume mwenye miaka 19, kuhusiana na mgomo ulio ibuka baada ya shambulizi hilo. Kamishna wa Polisi Karen Webb amesema mashtaka zaidi yanatarajiwa kufunguliwa kuhusiana na mgomo huo katika siku zijazo.

Kiongozi wa New South Wales Chris Minns amesema kufunguliwa tena kwa soko la Westfield Bondi Junction, ni fursa yaku yakutafakari kama jumuiya. Soko hilo limefunguliwa tena leo Aprili 18, sikwa sababu zakibiashara ila kwa siku ya jumuiya kutafakari nakuruhusu umma kutoa heshima zao kwa waathiriwa sita wa shambulizi baya la kisu la Jumamosi Aprili 13. Kiongozi wa NSW na kamishna wa Polisi Karen Webb, awali walitembelea soko hilo. Mkesha kwa mishumaa utafanywa katika Fukwe ya Bondi jumapili hii mida ya saa kumi na moja unusu kwa masaa ya mashariki Australia. Bw Minns amesema ni fursa kwa jumuiya kuja pamoja

Data kutoka shirika la usafiri wa anga la Flight Aware imeonesha zaidi ya safari 270 kutoka nakuingia uwanja wakimataifa wa ndege wa Dubai zime futwa, na zingine 370, zime cheleweshwa kwa sababu ya barabara ya ndege zilizo furikwa siku ya jumatano kwa masaa ya Dubai. Uwanja huo wa ndege umewashauri wasafiri wasiende huko kwa sababu ya mazingira yanayo zua changamoto, na mamlaka imeonya kuwa “itachukua muda kurejea katika hali ya kawaida”. Mvua kubwa katika mataifa ya Ghuba, ime uwa idadi ya takriban watu 20.
Dhoruba ya ziada, mvua nyingi pamoja na upepo Mkali una endelea kutabiriwa.

Serikali ya Burundi na Umoja wa Mataifa wameanzisha mchakato wa kuomba msaada wa ufadhili wa fedha ili kukabiliana na athari mbaya za mvua kubwa zinazonyesha kwa miezi kadhaa ambazo zimewakosesha makazi takriban watu 100,000. Taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa likishuhudia mvua kubwa katika wiki za hivi karibuni ambazo zimesababisha vifo vya watu 58 nchini Tanzania katika nusu ya kwanza ya mwezi Aprili, na watu 13 nchini Kenya. Burundi ambayo Umoja wa mataifa unasema ni moja ya nchi 20 zilizo katika hatari kubwa ya kukabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa, imekumbwa na mvua zinazonyesha karibu kila siku tangu mwezi Septemba, huku mji mkuu Bujumbura ukiharibiwa na mafuriko.

Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia maswala ya haki za binadamu, Volker Turk amezitembelea kambi za watu waliokoseshwa makazi kaskazini mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katika ziara yake ya siku tatu Voleker anatarajiwa kuwa na mikutano na watetezi wa haki za binadamu na mashirika ya jumuiya ya kiraia pamoja na rais Felix Tshisekedi na wajumbe wa serikali. Volker alitembelea maeneo yaliyokumbwa na mashambulizi ya karibuni yakishutumiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo wa ADF linalojihusisha na Islamic state ambapo karibu raia 10 hadi 15 waliuwawa mwishoni mwa wiki `katika wilaya ya Beni.

Wanawake tisa waliokamatwa nchini Zimbabwe kwa madai ya kumzomea mke wa rais Auxillia Mnangagwa wameondolewa mashtaka, vyombo vya habari vimeripoti. Mashtaka hayo yaliondolewa kufuatia agizo la Bi Mnangagwa, ripoti hizo jzikasema zikimnukuu msemaji wa rais George Charamba jana.
“Mama wa taifa na kamishna wa polisi wamekubaliana kwamba maafisa wahusika walichukua hatua ambayo haikuhitajika,” Bw Charamba akasema.

Katika michezo,
Utayari wa mji wa Brisbane kuwa mwenyeji wa michezo ya
olimpiki ya 2032, umehojiwa katika kikao cha seneti kwa maandalizi ya michezo ya Olimpiki jimboni Queensland. Meya wa zamani wa Brisbane, Graham Quirk alieleza kikao hicho kuwa hakuwa na taarifa kuhusu mipango ya serikali ya jimbo kutumia vifaa vya Queensland Sport and Athletics Centre [[QSAC]] sehemu yakufanyia baadhi ya michezo badala yakupendekeza kujenga uwanja mpya wa michezo.

Na katika utabiri wa hewa: 

Adelaide nyuzi joto ni, 19

Brisbane nyuzi joto ni, 28

Canberra nyuzi joto ni, 21

Darwin nyuzi joto ni, 34

Hobart nyuzi joto ni, 19

Perth nyuzi joto ni, 32

Melbourne nyuzi joto ni, 17

Sydney nyuzi joto ni 24

Share