Taarifa ya Habari 5 Machi 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili.jpg

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Anthony Albanese anatarajiwa kuweka wazi sera mpya zakupiga jeki ushiriki wa biashara za Australia, katika ukanda wa Kusini mashariki Asia, kongamano la ASEAN linapo anza leo mjini Jumanne Machi 5 mjini Melbourne.


Baraza la Saratani la Victoria limezindua kampeni mpya inayo zingatia umuhimu wa uchunguzi wa mara kwa mara wa uchunguzi wa kizazi. Kampeni kwa jina la In Your Hands, imejiri wakati data mpya kutoka sajili ya saratani ya Victoria, inaonesha kuwa zaidi ya watu 200 wa Victoria walitambuliwa kuwa na saratani ya kizazi katika mwaka wa 2022, na zaidi kesi 1000 zilitambuliwa katika miaka mitano kuanzia 2018 hadi 2022.

Udhibiti wa kulazimishwa na sheria za idhini ya uthibitisho, zita jadiliwa ndani ya bunge la Queensland leo Jumanne 5 Machi. Ziki pitishwa, sheria hizo zitawasilisha mfumo wa uthibitisho wa idhini na kuharamisha kuchezea ua kuondoa mpira wa kujamiana bila ridhaa- hatua inayo itwa kuiba. Geuzi hilo lita weka Queensland kuwa sawa na mamlaka zingine, isipokuwa Wilaya ya Kaskazini na Magharibi Australia.

Uchunguzi ume zinduliwa kwa madai kuwa vilipuzi vili lipuliwa chini ya wafanyakazi watatu ndani ya mgodi wa chini ya ardhi jimboni Queensland.

Majaji kwa kauli moja walibatilisha uamuzi wa mahakama ya juu ya Colorado kumuondoa Trump katika karatasi la upigaji kura. Mahakama ya juu nchini Marekani imempa Donald Trump ushindi mkubwa Jumatatu wakati akifanya kampeni kurejea tena kwenye urais ikibatilisha uamuzi wa mahakama ambao ulimuengua kutoka katika kura ya Colorado chini ya kifungu cha katiba kinachohusisha uasi kwa kuchochea na kuunga mkono shambulio la Januari 6 mwaka 2021 kwenye jengo la bunge la Marekani.

Maelfu ya wafungwa walitoroka Gereza la Taifa la Haiti, lililopo katika mji mkuu, wakati wa makabiliano ya bunduki usiku wa kuamkoa Jumapili, kati ya polisi wa kitaifa na makundi yenye silaha. Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry yuko nje ya nchi kwa sasa. Alienda wiki iliyopita nchini Kenya, ambapo alisaini makubaliano ya pande mbili kuruhusu maafisa 1,000 wa polisi wa Kenya ambao wataongoza kikosi cha usalama cha kimataifa.

Wataalamu wanaohusika na masuala ya amani na usalama pamoja na kukabiliana na migogoro wanakutana kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, kutathmini njia za kumaliza mizozo iliyopo kati ya nchi wanachama wa Kanda ya Maziwa Makuu na machafuko ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Albert Shingiro, ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa nchi 13 za Kanda ya Maziwa Makuu na Afrika Kusini zilizotia saini na Kongo amesema licha ya mkataba huo kutiwa saini zaidi ya miaka kumi sasa, kuna changamoto zinazo kwamisha utekelezaji wake.



Share