Taarifa ya Habari 8 Machi 2024

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya shirikisho imetoa ripoti yake ya pili ya mwaka kwa hali ya Wanawake, ripoti hiyo inaonesha pengo la malipo ya jinsia iko katika kiwango cha chini kwa asilimia 12 ila tofauti zingine kubwa zimesalia.


Ripoti hiyo, iliyo chapishwa katika siku ya kimataifa ya wanawake tarehe 8 Machi, ina onesha kuwa Australia iko katika nafasi ya 26 duniani kwa usawa wa jinsia kutoka nafasi ya 43 katika ripoti ya 2023.

Wakati Adelaide ina jiandaa kukabiliana na hali ya joto, mamlaka wame wahamasisha wanao hudhuria tamasha wazingatie usalama wanapo burudika katika tamasha kadhaa mjini humo. Ofisi ya utabiri wa hewa imetabiri nyuzi joto zitafika zaidi ya arobaini katika siku zijazo katika sehemu nyingi za jimbo la Kusini Australia. Tamasha ya WOMADelaide, ambayo ina anza leo usiku katika eneo la Botanic Park mjini Adelaide, imesema vivuli vya ziada pamoja na mabomba yaku nyunyuzia maji yata tolewa kwa watakao hudhuria tamasha hizo.

Wakulima wa Australia wanaomba sheria kali zaidi kwa masoko wakati uchunguzi wa bunge unatazama bei katika sekta hiyo. Tume ya Australia ya ushindani na watumiaji, ina fanya tathmini itakayo dumu kwa mwaka mmoja kwa sekta ya mboga, itachunguza uwekaji wa bei na uhusiano kati ya bei za jumla na reja reja. Wakulima wana omba adhabu kali kwa masoko yanayo zidisha malipo kwa watumiaji, wakati wanapunja wakulima kwa mauzo yao.

Ramadan ita anza nchini Australia tarehe 12 Machi. Mwanzo wa mwezi mtukufu wa Waislamu, hutegemea mwezi mpya unapo onekana mara ya kwanza. Baada ya ushauriano wa kina nama Imam wa baraza la Fatwa la Australia, kiongozi mkuu wa dini laki Islamu wa Australia Dr Ibrahim Abu Mohamad ametangaza kuwa siku ya kwanza ya mfungo itakuwa Machi 12. Usiku wa kwanza na Sala ya Taraweeh, itakuwa baada ya jua kutua tarehe 11 Machi.

Afrika Kusini imewasilisha ombi la haraka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya ICJ, kuiamuru Israel kukubali misaada zaidi ya kibinaadamu katika Ukanda wa Gaza, huku ikitahadharisha juu ya kitisho cha baa la njaa. Tangu kuanza kwa mapigano kati ya Israel na Hamas mnamo Oktoba 7, Wapalestina zaidi ya 30,000 wameuwawa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Ufaransa itabakisha wanajeshi wake nchini Chad, iliyo chini ya urawala wa kijeshi, huku ikiwaondoa kwingineko barani Afrika, kutokana na mvutano na tawala za kijeshi, mjumbe wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Alhamisi. Takriban wanajeshi 1,000 wa Ufaransa wanapiga kambi nchini Chad, ikiwa idadi ndogo ya wanajeshi katika nchi mshirika inayoongozwa na Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno tangu mwaka wa 2021.

Aliyekuwa mgombea wa Urais nchini Kongo Daktari Denis Mukwege, ameonya kuhusu kile anachodai ni hatari ya kujiondoa haraka kwa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO, mashariki mwa nchi hiyo. Mukwege anahofia kuwa hali hii huenda itakuwa mbaya kwa usalama wa raia na utulivu, na hivyo kuyafanya mafanikio ya miaka ishirini na mitano ya kuwepo kwa MONUSCO kupotea bure.






Share